Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Tafsiri ya Ulimwengu Mpya (kwa KiingerezaNew World Translation of the Holy Scriptures) ni tafsiri ya Biblia inayotolewa na Mashahidi wa Yehova.

. . . Tafsiri ya Ulimwengu Mpya . . .

Kabla ya mwaka1950 Mashahidi wa Yehova walitumia tafsiri nyingine zilizopatikana. Ilhali wanaamini ya kwamba makanisa yote yana kasoro nyingi[1] hawakutaka kutegemea tena vitabu vyao, hivyo walianza kutengeneza tafsiri ya kwao wenyewe kwa lugha ya Kiingereza. Agano Jipya lilipatikana mwaka 1950 na sehemu za Agano la Kale zilifuata hadi kukamilika mnamo mwaka 1960.

Tafsiri hiyo ya Kiingereza, si Biblia katika lugha zake asili (Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki), ndio msingi wa matoleo kwa lugha nyingine zote ili kuhakikisha umoja wa madhehebu yao duniani kote.

Dibaji ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya Kiswahili inaeleza kuwa “Toleo hili la Kiswahili la mwaka wa 2017 ambalo ndilo la karibuni zaidi limerekebishwa kwa kutegemea Biblia ya Kiingereza ya Tafsiri ya Ulimwengu Mpya iliyorekebishwa mwaka wa 2013”.[2]

Tabia kuu ya pekee ya tafsiri hiyo ni matumizi ya jina “Yehova” si tu kila mahali ambako Biblia ya Kiebrania inatumia YHWH lakini pia katika sehemu za Agano Jipya[3] ambapo jina hilo halipo, ila imeandikwa kwa KigirikiMungu au Bwana.

Kwa jumla wataalamu wa lugha na Biblia nje ya Mashahidi wa Yehova hukubaliana ya kwamba ni kosa kutamka YHWH kama “Yehova”[4].

Pamoja na hayo, wataalamu wengi wakikubaliana ya kwamba tafsiri hii kwa kawaida inatumia Kiingereza kizuri[5] bado kuna mifano mbalimbali ya kwamba matini ya Biblia ilibadilishwa kwa kusudi la kuthibisha mafundisho ya Mashahidi wa Yehova, hasa pale ambapo suala la Yesu kuitwa Mungu linaguswa.

Mifano miwili ni

  • katika Yohane 1:1 Kigiriki kinasema: “ὁ λόγος ἦν πρὸς τὸν θεόν, καὶ θεὸς ἦν ὁ λόγος”. Hapa tafsiri ya Union Version kwa kukubaliana na maneno ya Kigiriki inasema “Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya inatumia hapa “Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa mungu.” Kuhusu Yesu inatumia “mungu” kwa herufi ndogo ili kuonyesha mafundisho yao ya kwamba Yohane hakutaka kumtaja Neno (=Kristo) kuwa “Mungu” sawa na Muumba wa mbingu na nchi bali kama “mungu” mmojawapo chini yake. Kwa Kiingereza tafsiri inatumia “a god” badala ya “God”.
  • 2 Petro 1:1 Kigiriki kinasema: δικαιοσύνῃ τοῦ θεοῦ ἡμῶν καὶ σωτῆρος Ἰησοῦ Χριστοῦ; Kiswahili cha Union Version hapa ni: “haki ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo”. Tafsiri ya Ulimwengu Mpya inasema hapa “uadilifu wa Mungu wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo”; inaongeza “wetu” mara ya pili kwa kufuata mafundisho yao ya kwamba “Mungu” na “Yesu Kristo” ni wawili tofauti.[6]

. . . Tafsiri ya Ulimwengu Mpya . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Tafsiri ya Ulimwengu Mpya . . .

Previous post Renato Kizito Sesana
Next post Ifigenia wa Ethiopia