
More Than Words
“More Than Words” ni wimbo ulioimbwa na wanamuziki wanaoimba muziki wa wa midundo ya Rork wa kundi la Extreme. Mpiga gitaa katika wimbo huu anaitwa Nuno Bettencourt na sauti zimetiwa na Gary Cherone (na sauti za huruma kutoka kwa Bettencourt). Wimbo huu ulitoka mwaka 1990 katika albamu yao ya Extreme II: Pornograffiti.
. . . More Than Words . . .
Wimbo wenyewe unajaribu kumuuliza mlengwa kuonesha upendo wake zaidi ya maneno.
Tarehe 23 Machi mwaka 1991wimbo wa “More Than Words” uliingia katika chati ya Marekani ya Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya 81 na baada ya muda tu, ukawa tayari umeshafika katika nafasi ya kwanza. Pia ulifika katika nafasi ya pili katika chati ya muziki ya nchini Uingereza ambako kundi hili lilikuwa na mafanikio kabla ya kuingia katika soko la Marekani. Japokuwa walishawahi kufanya vizuri katika chati mbalimbali za nchini Marekani lakini wimbo huu ndio uliowafikisha juu zaidi katika chati za muziki za Marekani
Wimbo wa “More Than Words” ulifuatiwa na wimbo mwingine wa “Hole Hearted” ambao kidogo ulikuwa na mapigo ya haraka kuliko “More Than Words” lakini hata hivyo uliweza kufika katika nafasi ya 4, nchini Canada.
- Westlife mwaka 1999, katika albamu yao ya Westlife.
- David Cassidy mwaka 2003 katika albamu ya A Touch of Blue.
- Naturally 7 mwaka 2003 katika moja ya nyimbo katika albamu ya What is It?.
- Owen mwaka 2004, katika albamu ya nchini Japan ya I Do Perceive.
- Frankie J in 2005, kama single ya tatu kutoka katika albamu yao ya The One.
- Aloha Sex Juice aliumba nchini Hawaiian katika filamu ya mwaka 2008 Forgetting Sarah Marshall.
- Ruben Studdard aliurudia wimbo huu katika albamu yake ya mwaka 2009 ya Love Is.
- Owenaliurudia katika albamu ya “The Seaside EP” iliyotoka mwezi Julai 2009.
. . . More Than Words . . .