Mkoa wa Lindi

Lindi ni jina la mji, wilaya na mkoa ulioko Kusini-Mashariki mwa Tanzania.

Mahali pa Mkoa wa Lindi katika Tanzania

Mkoa wa Lindi ni kati ya mikoa 31 iliyopo nchini Tanzania yenye postikodinamba 65000.

Umepakana na mikoa ya Pwani, Mtwara, Ruvuma na Morogoro. Upande wa mashariki hupakana na Bahari Hindi.

. . . Mkoa wa Lindi . . .

Mkoa huu umeanzishwa mwaka 1971 na una eneo la km² 67,000. Karibu robo ya eneo lake au km² 18,000 ni sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous.

Mkoa una wilaya sita za: Lindi Mjini, Mtama (hadi 2019 Lindi Vijijini), Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa.

Mito mikubwa ndiyo Lukuledi, Matandu na Mavuji, yote yaelekea Bahari Hindi.

Mwinuko huanza mwambaoni ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu.

Mwaka 2002 idadi ya wakazi ilikuwa 791,306. Karibu asilimia 90 kati hao ni wakulima.

Makabila makubwa zaidi ni Wamwera, ambao wanapatikana hasa wilaya ya Nachingwea na Lindi vijijini katika kata za Rondo, halafu Wamachinga, Wamalaba ambao wako zaidi Lindi mjini, Wamatumbi na Wangindo huko Kilwa.

Wakazi kwa wilaya ni (idadi katika mabano): Kilwa (171,850), Lindi Mjini (41,549), Lindi Vijijini (215,764), Liwale (75,546), Nachingwea (162,081), Ruangwa (124,516),

Hali ya hewa ya Lindi ni ya joto mwaka wote ikiwa na wastani kati ya sentigredi 24,5 na 27.

Mkoa hupokea kati ya mm 980 na 1200 za mvua kwa mwaka, hasa kati ya miezi ya Novemba na Mei.

Kuna barabara chache katika hali nzuri. Ndizo km 155 za barabara ya lami na km 3567 za barabara ya mavumbi, mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Daressalaam imefungwa.

Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na jiji la Daresalaam tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji.

Kwa sasa barabara ya kutoka Mingoyo mpaka Dar es Salaam imekamilika kwa kiwango cha lami, kimebaki kipande cha kilometa 60 tu kuanzia Muhoro, wilaya ya Kilwa, mpaka kukaribia daraja la Mkapa juu ya mto Rufiji ambacho kinamaliziwa kwa kiwango cha lami.

Kuna kiwanja cha ndege Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia bandari. Huduma za simu zimepata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za mkononi.

Utalii haujafikia umuhimu sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu, ingawa Lindi ina sehemu mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa Kisiwani ndio mji wa kihistoria wa pwani ya Afrika ya Mashariki pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili, Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufuko wa mchanga ni wa kuvutia sana, nafasi za zamia majini ni tele.

Gesi iliyopatikana baharini karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo.

. . . Mkoa wa Lindi . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Mkoa wa Lindi . . .

Previous post VVU / UKIMWI nchini Angola
Next post Renato Kizito Sesana