Janette Deacon

Janette Deacon (née Buckland, alizaliwa Cape Town, 25 Novemba1939) ni mtaalam wa akiolojia wa Afrika Kusini aliyebobea katika usimamizi wa urithi na uhifadhi wa sanaa ya miamba. Amesomea mabadiliko ya zana za mawe kutoka maeneo ya kusini mwa Cape Town kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa miaka 20,000 iliyopita.[1][2] Kuanzia 1985, alipata maandishi ya mwamba mahali ambapo watoa habari wa / Xam Wilhelm Bleek na Lucy Lloyd waliishi katika karne ya kumi na tisa.[3]Alihudumu kama mshiriki wa Wakala wa Rasilimali za Urithi wa Afrika Kusini | SAHRA na alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Heritage Western Cape.

. . . Janette Deacon . . .

Janette Buckland alisomea shule ya wasichana ya Rustenburg huko Cape Town kabla ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town (UCT) mnamo mwaka 1960 na BA, ikifuatiwa na MA mnamo 1969 na PhD mnamo 1982 ambayo alichambua mkusanyiko wa baadhi wa zana za mawe (Stone Age) kutoka Pango la Nelson Bay, Pango la Boomplaas na makazi ya Kangkara.[4][5]

Baada ya kuhitimu BA yake alifanya kazi kama msaidizi wa utafiti wa WJ Talbot katika Idara ya Jiografia huko UCT.[6]na kuhadhiri katika Idara ya Akiolojia mnamo mwaka1962 na kutoka 1972 hadi 1975.[4]Kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1988 alikuwa msaidizi wa utafiti katika Idara ya akiolojia katika Chuo Kikuu cha Stellenboschkutoka mwaka 1976 mpaka mwaka 1993[7]Amekuwa Katibu wa Heshima wa Jumuiya ya Archaeologist ya Afrika Kusini tangu mwaka 1997. Ndani ya mwaka 1989 aliteuliwa kama mtaalamu wa akiolojia katika National Monuments Council (Afrika Kusini na Namibia) | National Monuments Council (NMC), mpaka yeye alipostaafu mwaka 1999. Wakati huu aliwakilisha NMC katika Kikundi Kazi cha Sanaa na Utamaduni na timu ya uandishi wa Sheria Rasilimali za Urithi wa Kitaifa Namba 25 ya mwaka1999.

Baada ya kustaafu alikua mwenyekiti wa kwanza wa Heritage Western Cape (HWC) mnamo mwaka 2002 akihudumu hadi mwaka 2007[8]Kama katibu wa Mradi wa Sanaa ya Mwamba Kusini mwa Afrika, aliweka kozi na semina za uteuzi wa tovuti za sanaa za miamba kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia. Kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2011 mpango huu uliendelezwa zaidi kama mradi wa Getty Conservation Institute.

Mnamo 2016, alipewa udaktari wa heshima katika fasihi kutoka UCT kwa michango yake kwa akiolojia na utafiti wa sanaa ya miamba.[9]

. . . Janette Deacon . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Janette Deacon . . .

Previous post Justine Waddell
Next post VVU / UKIMWI nchini Angola