Frédéric Chopin

Frédéric Chopin (jina la Kipoland: Fryderyk ; 22 Februari1810 kulingana na cheti cha kuzaliwa – 17 Oktoba1849; pengine, tarehe 1 Machi au 10 Machi zimetajwa kama siku yake ya kuzaliwa) alikuwa mtunzi wa Opera na mpigaji kinanda mashuri kutoka nchini Poland. Ni mtunzi muhimu kabisa kwa nchi ya Poland. Ingawaje kuna baadhi ya tungo zake zilikuwa vigumu sana kuzipiga, na zilibahatika kuwa moja kati ya tungo zilizowahi kutungwa vema.

Frédéric Chopin.

Alizaliwa katika kijiji kidogo cha Żelazowa Wola karibu na Warshawa wakati sehemu ile ilikuwa chini ya utawala wa Urusi. Baba alikuwa Nicolas Chopin Mfaransa aliyeishi Poland kama mwalimu na mamake Justyna Krzyżanowska aliyetoka katika familia ya makabaila maskini wa Poland. Frederic alianza mapema kupiga kiananda akaonyesha uwezo mkubwa. Alipofikia umri wa miaka 20 alisafiri Ufaransa alipotoa maonyesho ya muziki yake. 1830 baba alimshauri asirudi Poland kwa sababu ya uasi wa Wapoland dhidi ya utawala wa Kirusi. Baada ya kukandamizwa kwa uasi huu Frederic alibaki nje ya nchi yake ya kuzaliwa akaendelea kuishi na kufanya kazi mjini Paris hasa.

Ni hapa Paris ya kwamba alikuwa maarufu kama mtunga muziki. Alianzisha mapenzi na wanawake mbalimbali lakini hakubahatika kufunga ndoa. Afya yake ilikuwa hafifu muda wote akafa mjini Paris kwa sababu ya ugonjwa wa kifua kikuu mwaka 1849 akiwa na umri wa miaka 39 pekee. Alizikwa Ufaransa lakini moyo wake ulipelekwa Poland na kuzikwa huko katika kanisa mjini Warshawa.

. . . Frédéric Chopin . . .

  • Chopin MusicArchived 20 Aprili 2008 at the Wayback Machine. – Website and forum dedicated to the music of Chopin, including recordings, sheet music and image galleries.
  • Chopin: the poet of the piano – A favourite Chopin place since 1999 with biography, images, complete music and score, discussion forum, work list and analysis, quizzes and contests, noted interpreters/great pianists…
  • Internet Chopin Information Centre, Chopin portal including calendar, catalogues, other information about Chopin, Chopin on the Web, and pianists’ biographical notes.
Wasifu
Tungo za muziki
Baadhi ya rekodi
Mengineyo
WikiMedia Commons

Orodha ya Wanamuziki wa kipindi cha Romatiki
AlkanBalakirevBeethovenBelliniBerliozBerwaldBizetBorodinBrahmsBrucknerChopinCuiDvořákElgarFieldFranckGlinkaGriegLisztMahlerMendelssohnMussorgskyRachmaninoffRimsky-KorsakovSaint-SaënsSchubertSchumannSmetanaStraussTchaikovskyVerdiWagnerWolfWeber

. . . Frédéric Chopin . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Frédéric Chopin . . .

Previous post Orodha ya milima ya Marekani
Next post Mapinduzi ya Zanzibar