Reli ya SGR ya Kenya

Reli ya SGR ya Kenya ni mfumo mpya wa reli nchini Kenya kati ya miji wa Mombasa na Nairobi unaotumia geji sanifu (kwa Kiingereza: standard gauge). Reli hiyo ni mradi mkubwa wa miundombinu tangu uhurumwaka1963. Ilijengwa na kampuni ya China Road and Bridge Corporation kwa kutumia wajenzi kutoka China pamoja na Wakenya 25,000 katika muda wa miaka mitatu hadi mwaka 2016.[1]

Reli ya SGR huko Kenya

Urefu ya reli ya SGR ya Kenya ni kilomita 472 na kuna stesheni tisa.

Stesheni
Mombasa Terminus
Mariakani
Miasenyi
Voi
Mtito Andei
Kibwezi
Emali
Athi River
Nairobi Terminus

. . . Reli ya SGR ya Kenya . . .

Reli ya zamani ya Kenya ilijengwa wakati wa ukoloni. Ilikuwa hasa njia ya Reli ya Kenya-Uganda. Iliporomoka tangu mwaka 2000 kwa sababu ya ukosefu wa matengenezo. Treni ya abiria ilihitaji siku nzima kutoka Mombasa hadi Nairobi badala ya saa 12 jinsi iliovyokuwa katika miaka ya 1990. Serikali ya Kenya ilikubali kukodi makandarasi ya Kichina kujenga reli ya kisasa wakati wa 2011.[2] Mradi huo umekamilishwa wakati wa mwezi Desemba mwaka 2016, takriban miezi 18 mapema zaidi.[3]


Watu wanaweza kusafiri mpaka bandari ya Mombasa au hadi mji mkuu Nairobi kwa urahisi sasa kwa sababu ya reli mpya. Watahitaji kutumia saa nne na nusu tu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi. Bila shaka, reli mpya itapunguza muda wa kusafiri. Kisha, ajali zimezidi barabarani kwa sababu ya kuongezeka kwa magari. Watu wanataka kutumia reli kwa sababu ya usalama pia.

Ujenzi wa reli ya Standard Gauge ya Kenya umeongeza nafasi za kazi kwa watu elfuishirini na tano Wakenya kulingana na mkataba kati ya serikali ya Kenya na makandarasi ya China.[4]Vijana wenyeji wengi wamepata seti mpya ya ujuzi kutokana na mradi huu. Inawezekana kwamba vijana wa Kenya wanaweza kupata kazi nzuri baada ya kukamilishwa kwa ujenzi wa reli kwa sababu ya ujuzi ambao walisoma. Reli ya kisasa itaongeza kazi, kama wahudumu katika treni, na wauzaji katika stesheni.

Treni ya SGR kwenye kituo cha Nairobi

. . . Reli ya SGR ya Kenya . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Reli ya SGR ya Kenya . . .

Previous post Barabara ya hariri
Next post Albert Batyrgaziev