Lazaro wa Serbia

article - Lazaro wa Serbia

Lazaro Hrebeljanović (kwa Kiserbokroatia Лазар Хребељановић; 1329 hivi – 15 Juni1389) alikuwa mtawala mkuu wa Serbia baada ya Dola la Serbia kusambaratika, akimiliki mabeseni ya mito Morava: Morava kuu, Morava magharibi na Morava kusini tangu mwaka 1373 hadi kifo chake vitani.

Lazaro alivyochorwa (Monasteri ya Ravanica, miaka ya 1380).

Kwa msaada wa Kanisa la Kiorthodoksi la Serbia alijaribu kufufua dola hilo, lakini watawala wengine wa taifa hilo hawakumkubali.

Hatimaye Lazaro aliuawa katika Mapigano ya Kosovo alipoongoza jeshi la Wakristo dhidi ya lile la Dola la Osmani, lililoongozwa na SultaniMurad I.

Wakristo walishinda, lakini walikufa kwa wingi, kiasi kwamba mwaka uliofuata mjane wa Lazaro alikubali himaya ya Waosmani.

Lazaro anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifumfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe28 Juni.

. . . Lazaro wa Serbia . . .

    . . . Lazaro wa Serbia . . .

    This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

    . . . Lazaro wa Serbia . . .

    Previous post Kipululu
    Next post Ubepari