Kitabu cha Ezra

Kitabu cha Ezra kinapatikana katika Biblia ya Kikristo katika Agano la Kale.

Koreshi Mkuu akiruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka Babuloni (mchoro mdogo wa Jean Fouquet, 14701475 hivi).

Kiasili kiliandikwa kwa lugha ya Kiebrania lakini kuna pia sehemu fupi za Kiaramu.

Andiko la Ezra lilitunzwa katika Biblia ya Kiebrania pamoja na Nehemia kama kitabu kimoja lakini kimegawiwa baadaye kuwa vitabu viwili ambavyo Vulgata inavitaja kama “Esdras I” na “Esdras II”.

Kitabu kinasimulia habari za Wayahudi chini ya utawala wa Waajemi.

Mwaka 587 KKmfalme wa Babeli alikuwa amevamia mji wa Yerusalemu, kubomoa hekalu la Sulemani na kumaliza ufalme wa Yuda. Wakazi walipelekwa Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Tangu wakati huo Waisraeli kwa kawaida walijulikana kuwa Wayahudi. Lakini, kwa kuwa utengano wa Israeli haukuendelea, majina hayo mawili, pamoja na jina la Waebrania, yaliweza kutumiwa kwa watu walewale (Yer 34:9; Yn 1:19, 47; 2 Kor 11:22; Gal 2:14).

Mwaka 539 KKWaajemi chini ya mfalme Koreshi walivamia Babeli ambayo ikawa jimbo la milki ya Uajemi. Koreshi aliwaruhusu Wayahudi kadhaa warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu.

Habari hizi na zilizofuata zinasimuliwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

. . . Kitabu cha Ezra . . .

Inaonekana vitabu vya Mambo ya Nyakati, Ezra na Nehemia viliandikwa kama mfululizo wa habari. Ndiyo sababu habari za Ezra zinaanzia wakati uleule ambapo habari za Mambo ya Nyakati zinamalizika.

Wakati huo ulikuwa mwaka 538 KKWaajemi walipokuwa wameshinda Babeli muda mfupi uliopita, na mfalme wao Koreshi, alikuwa ametangaza amri iliyowapa Wayahudiuhuru wa kurudi katika nchi yao (2 Nya 36:22-23; Ezra 1:1-4).

Wakati uliofuata unajulikana kuwa wakati wa baada ya uhamisho wa Babeli. Vitabu kadhaa vya Biblia (vya historia na vya manabii), vinahusika na wakati huo. Muhtasari wa matukio unaotolewa hapa chini unataka kusaidia kuelewa vitabu hivyo zaidi.

Miaka kama 200 hivi ya nyuma watu wa ufalme wa kaskazini walipelekwa kifungoni katika mataifa mbalimbali, wengi wao wakapoteza utambulisho wa taifa lao. Lakini watu wa ufalme wa kusini, yaani wa Yuda, walipopelekwa Babeli baadaye, walihifadhi utambulisho huo.

Kufuatana na amri ya Koreshi ya mwaka wa 538 KK, Wayahudi walirudi Yerusalemu kwa maelfu. Walikuwa na viongozi wao wa Kiyahudi, yaani Zerubabeli aliyekuwa kiongozi tangu wakati wa kifungoni, na kuhani mkuuYoshua, lakini wote waliendelea kuwa chini ya himaya ya Uajemi, hivyo walikuwa chini ya wafalme wake. Mji wa Yerusalemu ulikuwa katika mkoa uliojulikana kuwa “Ng’ambo ya Mto” (au “Magharibi ya Frati”), ulioanza katika Mto Frati na kuendelea mpaka Bahari ya Kati (Ezra 4:10, 16; 7:21, 25).

Muda mfupi baada ya kufika Yerusalemu, Wayahudi walianza kazi ya kujenga hekalu upya. Madhabahu iliwekwa mahali pake tena, na katika mwaka wa pili misingi ya hekalu ikawekwa (Ezra 3:1-3, 8-10). Lakini wakati huo maadui walianza kuwapinga wajenzi wakasababisha kazi yote iahirishwe kwanza (Ezra 4:1-5, 24).

. . . Kitabu cha Ezra . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Kitabu cha Ezra . . .

Previous post Watawala wa Ethiopia
Next post Esthete