Kipululu

-Kwa kiunzi cha binadamu tazama makala “Kiunzi cha mifupa“-

Kipululu

Kipululu wa Afrika (Turnix sylvaticus lepurana)

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Turnicidae (Ndege walio na mnasaba na vipululu)
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 17:

 • OrtyxelosVieillot, 1825
  • O. meiffrenii
 • TurnixBonnaterre, 1791
  • T. castanotus(Gould, 1840)
  • T. everettiHartert, 1898
  • T. hottentottus(Temminck, 1815)
  • T. maculosus(Temminck, 1815)
  • T. melanogasterGould, 1837
  • T. nanus(Sundevall, 1850)
  • T. nigricollis(Gmelin, 1789)
  • T. ocellatus(Scopoli, 1786
  • T. olivii(Robinson, 1900)
  • T. pyrrhothorax(Gould, 1841)
  • T. suscitator(Gmelin, 1789)
  • T. sylvaticusDesfontaines, 1789
  • T. tankiBlyth, 1843
  • T. varius(Latham, 1801)
  • T. velox(Gould, 1841)
  • T. worcesteriMcGregor, 1904

Vipululu (pia vipururu) ni ndege wa familiaTurnicidae. Spishi moja inaitwa kiunzi pia (tazama orodha ya spishi). Ndege hawa wanafanana tombo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana rangi ya mchanga na madoa meusi au kahawia. Hawapendi kupuruka. Jike ana rangi kali kuliko dume na huanzisha ubembelezi. Dume huatamia na hutunza makinda.

Ndege hawa waliainishwa zamani ndani ya Gruiformes (oda ya makorongo) au Galliformes (oda ya kuku). Lakini utafiti wa ADN umeonyesha kama vipululu wana mnasaba na vitwitwi. Kwa hivyo wanaainishwa ndani ya Charadriiformes sasa. Kisukuku kimefunuliwa ambacho kimetambuliwa kama jamaa wa vipululu na kuitwa Turnipax.

. . . Kipululu . . .

. . . Kipululu . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Kipululu . . .

Previous post Orodha ya makala za afya na magonjwa
Next post Lazaro wa Serbia