Hati ya Thesalonike

Hati ya Thesalonike (maarufu pia kwa jina la Cunctos populos) ilitolewa tarehe 27 Februari380BK. Iliagiza raia wote wa Dola la Roma kukiri imani ya maaskofu wa Roma na Aleksandria, ikifanya Ukristo wa Kikatoliki kuwa dini rasmi ya dola hilo.[1]

. . . Hati ya Thesalonike . . .

KaisariKonstantino I aliongokea Ukristo mwaka 312.

KUfikia mwaka 325uzushi wa padriArio kuhusu Yesu Kristo ulikuwa umeshaenea kiasi cha kuvuruga Kanisa na hata jamii nzima.

Ili kurudisha amani katika dola, Konstantino aliitisha Mtaguso wa kwanza wa Nisea ili uamue imani sahihi ni ipi. Mtaguso mkuu huo ulitoa Kanuni ya imani ya Nisea iliyokanusha Uario kwa kumkiri Kristo kuwa “Mungu kweli” mwenye “hali moja na Baba“.[2]

Hata hivyo mabishano hayakuisha, hivyo Konstantino alidhani amekosea kuunga mkono imani ya Nisea akasimama upande wa Waario akivuta wengi upande huo. Hatimaye, alipobatizwa (337), alimchagua askofu wa Kiario Eusebio wa Nikomedia kumbatiza.[2]

Mrithi wake upande wa mashariki, mwanae Constantius II, alikuwa vilevile mtetezi wa Uario akawa anafukuza maaskofu Wakatoliki.

Mwandamizi wake Kaisari Juliani aliasi kabisa Ukristo na kurudia Upagani wa Ugiriki, pamoja na kulinda dini na madhehebu yoyote.

Aliyemfuata, Kaisari Joviano, alitawala miezi 8 tu, akafuatwa na Kaisari Valens, muumini wa Uario.[2]

Mwaka 379, Valens aliporithiwa na Theodosius I, Uario ulikuwa umeenea sana mashariki, lakini si magharibi. Theodosius, aliyezaliwa Hispania, alikuwa na imani kubwa katika mafundisho ya Nisea. Mnamo Agosti, Gratian, mtawala wa magharibi, alianza kudhulumu wazushi.[2]

. . . Hati ya Thesalonike . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Hati ya Thesalonike . . .

Previous post Choo cha shimo
Next post Kwale (ndege)