
Choo cha shimo
.jpg/475px-Defecating_into_a_pit_(schematic).jpg)
Choo cha shimo au choo cha zamani ni aina ya choo ambapo kinyesi cha binadamu hukusanywa kwenye shimo ardhini.
. . . Choo cha shimo . . .
Vyoo hivi havitumii maji au hutumia kati ya lita moja na tatu kwa kila mara ya utumiaji kwa vyoo vya shimo vinavyotumia maji ya kumwangwa.[2] Vikijengwa na kudumishwa vyema, vinaweza kupunguza kuenea kwa magonjwa kwa kupunguza kiasi cha kinyesi cha binadamu kwenye mazingira kutokana na kwenda choo mahali wazi.[3][4] Hii hupungza usambazaji wa vimelea kutoka kwa kinyesi hadi chakula unaosababishwa na nzi.[3] Vimelea hivi ni visababishi vikuu vya maambukizi ya kuharisha na maambukizi wa minyoo ya utumbo.[4] Maambukizi ya kuharisha yalisababisha takriban vifo milioni 0.7 vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano mwaka wa 2011 na watoto milioni 250 walikosa kwenda shuleni siku kadhaa.[4][5] Vyoo vya mashimo ni mbinu ya gharama ya chini zaidi ya kuhakikisha kinyesi kimeondolewa karibu na watu.[3]
Kwa kijumla, choo cha shimo huwa na sehemu tatu: shimo la ardhini, sakafu iliyo na shimo dogo, na chumba kilicho na paa.[2] Kwa kawaida, shimo la ardhini huwa na kina cha angalau mita 3 (futi 10 ) na upana wa mita 1 (futi 3.2).[2]Shirika la Afya Duniani kinapendekeza vijengwe mbali kidogo na nyumba, kwa kuzingatia masuala ya harufu inayotoka chooni na ufikiaji wa urahisi.[3] Umbali na maji ya ndani ya ardhi na maji ya juu ya ardhi unafaa kuwa mkubwa iwezekanavyo ili kupunguza hatari ya uchafuzi. Shimo la sakafuni halifai kuzidi upana wa sentimita 25 (inchi 9.8) ili watoto wasije wakaanguka humo. Mwangaza haufai kuingia humo ili kuzuia inzi wasiingie. Jambo hili linaweza kuhitaji kutumia kifuniko kwenye shimo la sakafuni ikiwa halitumiki.[3] Choo kikishajaa hadi mita 0.5 (futi 1.6) karibu na sehemu ya juu, kinafaa kuondolewa kinyesi chote au choo kipya kijengwe mahali tofauti.[6] Udhibiti wa maji maji ya kinyesi yaliyoondolewa chooni huwa tata. Kuna hatari za kimazingira na kiafya yasipodhibitiwa vyema.
. . . Choo cha shimo . . .