
Sierra Leone
Sierra Leone ni nchi ya Afrika ya Magharibi.
Imepakana na Guinea na Liberia, upande wa magharibi iko bahari ya Atlantiki.
Jina la nchi lina asili ya Kireno na linamaanisha “Mlima wa Simba”.
Ni koloni la zamani la Uingereza na tangu 27 Aprili1961 ni jamhuri huru.
Sierra Leone ni kati ya nchi maskini sana duniani.
. . . Sierra Leone . . .
-
Makala kuu: Historia ya Sierra Leone
Nchi yenyewe ilianzishwa na Waingereza kwa kuunda mji wa Freetown (“Mji wa watu huru”) mwaka1787. Kusudi lake likuwa kuwarudisha Afrika watu waliowahi kuwa watumwa. Kiasili wale wakazi wa kwanza walikuwa watumwa weusi waliopewa uhuru kwa sababu walishikamana na Waingereza dhidi ya Wamarekani katika vita vya uhuru wa Marekani.
Baadaye Waingereza wapinzani wa utumwa walinunua watumwa wakiwapa uhuru na kuwapeleka Sierra Leone.
Tangu mwaka 1807Uingereza ulikataza biashara ya watumwa (lakini utumwa wenyewe bado) na watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara hiyo haramu walipelekwa Sierra Leone na kupewa uhuru.
Ikianzishwa na shirika la wapinzani wa utumwa Sierra Leone ikawa koloni la kwanza la Uingereza katika Afrika ya Magharibi mwaka 1792. Kuanzia mwaka 1802 Freetown ilikuwa makao makuu ya Kiingereza kwa Afrika ya Magharibi.
Mwaka 1961 Sierra Leone ilipewa uhuru wake.
Miaka 1994 – 2002 nchi ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu mwisho wake nchi inajengwa tena.
Wakazi asili wamegawanyika katika makabila 16, kila moja likiwa na lugha na utamaduni maalumu; kati yake makubwa zaidi ni Watemne (35%) na Watembe (31%).
Lugha inayojulikana na asilimia 90 za wakazi ni Kikrio, aina ya Krioli ya Kiingereza iliyochanganya pia lugha mbalibali za Kiafrika. Lakini lugha rasmi ni Kiingereza.
Upande wa dini, Waislamu ni 71-77%, Wakristo ni 21-27% na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika hawafikii 2%. Sierra Leone ni nchi isiyo na dinirasmi.
. . . Sierra Leone . . .