Mwana wa Mungu

Mwana wa Mungu” ni jina linalotumiwa katika dini mbalimbali ili kusisitiza uhusiano wa mtu fulani na Mungu au mmojawapo wa miungu. Kwa maana hiyo lilitumika hasa kwa ajili ya watawala.

Mungu Baba na Roho Mtakatifu pamoja na mtoto Yesu kadiri ya Murillo, 1670 hivi.

Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
YesuKristo na Ukristo

Umwilisho Utoto wa Yesu Ubatizo
Arusi ya Kana Utume wa Yesu Mifano ya Yesu Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura Karamu ya mwisho Msalaba wa Yesu Maneno saba
Kifo cha Yesu Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni Ujio wa pili
Injili Majina ya Yesu katika Agano Jipya Yesu kadiri ya historia Tarehe za maisha ya Yesu Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi Kiaramu Bikira Maria Yosefu (mume wa Maria) Familia takatifu Ukoo wa Yesu Ndugu wa Yesu Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya ·Mitazamo ya Kikristo Mitazamo ya Kiyahudi Mitazamo ya Kiislamu Yesu katika sanaa

Pengine linamaanisha viumbe vingine, kama vile malaika.

. . . Mwana wa Mungu . . .

Katika Biblia ya Kikristo jina hilo linamhusu kwa namna ya pekee sana Yesu, na katika madhehebu karibu yote ya Ukristo linafafanuliwa kumaanisha asili yake ya milele katika Mungu pekee kabla ya kujifanya binadamu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya Bikira Maria.[1]

Ukurasa wa kwanza wa Injili ya Marko: “Mwanzo wa habari njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu“, karne ya 14.

Kadiri ya Injili, Yesu Kristo mwenyewe alisisitiza mara nyingi uhusiano wake wa pekee na Baba wa mbinguni kutokana na asili yake toka juu, tofauti na ile ya watu wengine wote.

Kupaa Bwana kadiri ya Pietro Perugino (1500 hivi), Lyon, Ufaransa.

Kila mmoja kwa namna yake, Mtume Paulo, Wainjili na waandishi wengine wa Agano Jipya walitumia sana jina hilo, hata kuliweka pembeni kidogo jina lingine lililotumiwa sana na Yesu mwenyewe, yaani Mwana wa Adamu.

Jina hilo lilizidi kutafsiriwa kwa namna tofauti kadiri teolojia ilivyostawi, hasa baada ya kaisariKonstantino Mkuu kuruhusu Ukristo katika Dola la Roma (313).

Kutokana na fujo zilizojitoleza hata kuhatarisha amani ya dola, mwenyewe, akishirikiana na Papa Silvesta I, aliitisha mtaguso mkuuwa kwanza uliofanyika mwaka 325 huko Nisea.

Mtaguso huo ulitunga kanuni ya imani iliyokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa maana ana hali moja na Mungu Baba, hakuumbwa bali alizaliwa naye tangu milele yote.

Konstantino Mkuu na mababu wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea.

Wakristo wanapomkiri Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu… Amwaminiye yeye hahukumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yoh 1:1,14; 3:18).

. . . Mwana wa Mungu . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Mwana wa Mungu . . .

Previous post Nnenna Okore
Next post Audie Cornish