Kaswende

Kaswende (ing.syphilis) ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa ambayo inasababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum.

Kaswende – Syphilis
Mwainisho na taarifa za nje

Electron micrograph of Treponema pallidum
ICD10 A50.A53.
ICD9 090097
DiseasesDB 29054
MedlinePlus 000861
eMedicine med/2224emerg/563derm/413
MeSH D013587
Vipele vya awali vya kaswende katika uume.
Hatua ya pili ya kaswende inavyojitokeza mikononi.
Mfano wa kichwa cha mtu mwenye kaswende katika hatua ya tatu.

Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambavyo baadaye hupotea vyenyewe.

Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi huendelea kwa miaka, yakishambulia mifupa, ubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi.

Kaswende wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deformity) na kifo.

Wanawake wengi wajawazito katika nchi zilizoendelea huchunguzwa kwa uwepo wa ugonjwa huu katika majuma ya kwanza ya mimba ili kutibu ugonjwa kabla kitoto hakijaathirika.

Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi fulani kwa penicillin.

. . . Kaswende . . .

Kaswende inasababishwa na bakteria ya spirochete Treponema pallidum baadhi ya spishi pallidum. Njia ya kawaida zaidi ya kuambukizwa ni kupitia ngono; hata hivyo, kaswende pia inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama hadi kwa mimba wakati wa ujauzito au wakati wa kuzaliwa kwa mtoto, na kusababisha kuzaliwa na kaswende. Magonjwa mengine ya binadamu yanayohusiana niTreponema pallidumbakteria inajumusiha buba (baadhi ya spishi pertenue), pinta (baadhi ya spishi carateum) na bejel (baadhi ya spishi endemicum).

Dalili na ishara za kaswende hutofautiana kulingana na hatua iliyoko kati ya hatua nne. Hatua ni ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho. Hatua ya kwanza kawaida inajitokeza kimoja na shanka utokeaji wa kidonda kwa ngozi isiyowasha, ngumu, isiyokuwa na uchungu). Hatua ya pili ya kaswende hujitokeza na upele ambayo mara kwa mara inahusisha viganja vya mikono na nyayo za miguu. Hatua fiche ya kaswende hujitokeza na dalili kiasi au hata bila. Hatua ya mwisho ya kaswende hujitokeza na guma, dalili zinazohusiana na mfumo wa neva, au zinazohusiana na moyo.

Hata hivyo, kaswende imeitwa “mwiigaji mkuu” sababu mara nyingi hujitokeza kwa njia isiyo ya kawaida.

Kwa kawaida kaswende hutambulika kwa uchunguzi wa damu;hata hivyo, bakteria inaweza kuonekana kwa kutumia hadubini. Kaswende inaweza kutibiwa kwa njia inayofaa kwa kutumia antibiotiki, haswa ndani ya misuli penisilini G. Hii inapendekezwa kwa watu walio na aleji ya penisilini, seftriaksoni.

Inaaminika kwamba kufikia mwaka wa 1999 watu milioni 12 walikuwa wameambukizwa kaswende ulimwenguni na zaidi ya asilimia 90 ya hali hizi kutoka kwa nchi zinazoendelea. Hali za kaswende zilipungua kwa kasi baada ya penisilini kupatikana kwa urahisi katika miaka ya 1940, lakini viwango vya maambukizi vimeongezeka tangu mwaka 2000 katika nchi nyingi. Mara nyingi kaswende hupatikana pamoja na virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU). Hii imehusishwa na sehemu ya matendo ya ngono yasiyokuwa salama kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine;Ongezeka la uasherati; ukahaba; na kupungua kwa matumizi ya kondomu.[1][2][3]

Kaswende inaweza kuwa katika hatua moja kati ya hatua nne tofauti: ya kwanza, ya pili, fiche, na ya mwisho,[4] na pia inaweza kujitokeza wakati wa kuzaliwa.[5] ilirejelewa kama “mwiigaji mkuu” na Sir William Osler kutokana na njia mbalimbali inavyojitokeza[4][6]

. . . Kaswende . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Kaswende . . .

Previous post Milipuko ya Mabomu – Mbagala
Next post Orodha ya miji ya Uholanzi