Historia ya maeneo ya Pasifiki

Historia ya Maeneo ya Pasifiki inahusu historia ya watu kwenye visiwa vya Pasifiki. Historia hiyo huangaliwa kufuatana na kanda zake kama vile Polinesia, Melanesia na Mikronesia; mara nyingi historia inaangaliwa pamoja na Australia na Nyuzilandi(ing.History of Oceania).

Kanda ndani ya maeneo ya Australia na visiwa vya PAsifiki

. . . Historia ya maeneo ya Pasifiki . . .

Mtoto wa Vanuatu

Historia ya maeneo ya Pasifiki ilianza na uhamiaji wa wanadamu walioenea huko angalau miaka 40,000 iliyopita. Walitoka Asia ya Kusini-Mashariki wakafika Australia na Guinea Mpya pamoja na visiwa kadhaa vya Melanesia. Eneo kubwa la visiwa vilivyotawanyika katika Bahari Pasifiki lilikuwa halijakaliwa na watu bado.

Watu walianza kuenea huko mnamo 1500 KK1300 KK, uwezekano mkubwa ni kwamba walitokea mwanzoni Ufilipino na Taiwan. Katika mwendo wa karne nyingi wahamiaji walifikia kisiwa kimoja baada ya kingine na kupanua eneo la makazi zaidi upande wa mashariki.

Wapolinesia walifika kwenye pembetatu ya TongaFijiSamoa wakaendelea kwa safari za mbali wakiwa na mitumbwi yao hadi kufika Hawaii, Nyuzilandi na mashariki mwa Pasifiki hadi Kisiwa cha Pasaka.

Historia ya uenezi huo ni vigumu kuifanyia utafiti kwa sababu watu hao hawakuwa na maandishi. Ni mila chache tu za mdomo ambazo zimeendelea kuhifadhiwa hadi nyakati za kisasa, kama vile kuhusu makazi ya kwanza New Zealand yaliyoanzishwa na Tama Te Kapua. Taarifa zilizoandikwa zinapatikana tu tangu kufika kwa Wazungu wa kwanza katika karne ya 16.

Safari ya Magellan alipozunguka Dunia yote kwenye karne ya 16.

Katika karne ya 16 Wareno na Wahispania walikuwa Wazungu wa kwanza kusafiri katika Bahari Pasifiki. Waliwahi kufika Amerika kuanzia Kristoforo Kolumbus wakitafuta njia ya kufika China na Uhindi wakihamasishwa na shabaha za kibiashara na za kisiasa; walitaka kuanzisha biashara ya moja kwa moja na matajiri wa Mashariki bila kulazimishwa kulipa bei za juu za wafanyabiasharaWaislamu waliotawala biashara hiyo hadi wakati ule.

Mwisho wa karne ya 16 na katika karne ya 17 hao wakwanza walifuatwa na Waholanzi, Waingereza na Wafaransa.

. . . Historia ya maeneo ya Pasifiki . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Historia ya maeneo ya Pasifiki . . .

Previous post A New Day …
Next post Athroskopia