Edgar Ngelela

article - Edgar Ngelela

Edgar Leonard Luhende Ngelela (amezaliwa 15 Oktoba1980[1]) ni msanii katika masuala ya muziki, uchoraji, uigizaji, uongozaji wa michezo ya jukwaa na ya runingana utengenezaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Ikiwa na pamoja na kucheza maigizo bubu, muziki, kuchora, kubuni na kutengeneza filamu ametumia elimu yake katika kufundisha sehemu mbalimbali kama Chuo kikuu cha Dar es Salaam na TFTC.

Edgar Ngelela, 2012

Edgar Ngelela

Maelezo ya awali
Amezaliwa 15 Oktoba1980 (1980-10-15) (umri 40)
Kazi yake Mwimbaji, Mtunzi, Muigizaji, Muongozaji na mtengeneza Filamu

Mwaka 2013 Ngelela alitengeneza filamu fupi iitwayo ‘Anguko’ ambayo ilishirikikatika matamasha mbalimbali ya filamu. Haya ni pamoja na Tamasha la majahazi Zanzibar,Archived 21 Machi 2019 at the Wayback Machine.(The Zanzibar International film festival; ZIFF)Archived 21 Machi 2019 at the Wayback Machine.,na Arusha Afirican film festival (AAFF)Archived 17 Oktoba 2013 at the Wayback Machine..

. . . Edgar Ngelela . . .

Edgar Ngelela alizaliwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Tanzania. Akiwa mtoto wa hayati Felix Ngelela Luhende na mama Hildegald Lyimo Luhende, wazazi wake walihamia Mkoani Shinyanga akiwa bado mdogo. Huko walizaliwa wadogo zake: Nicholaus Ngelela Luhende na Benedict Ngelela (Bennysofar).

Alianza kusoma elimu ya awali maarufu kama vidudu, kabla ya kuanza darasa la kwanza mwaka 1987 katika shule ya msingi Mwenge, lakini mwaka huohuo alihamia katika shule ya kimataifa iliyoko mkoani Arusha inayoitwa Mtakatifu Constantine, ambako aliendelea hadi darasa la tatu, na badaye kutokana na hali ya hewa mkoani humo, ilimshinda Edgar kiafya. Hivyo, familia yake iliamua kumwamishia katika shule ya msingi ya Nyakahoja iliyoko mkoani Mwanza, ambapo ndipo alipomalizia elimu yake ya msingi.

Baada ya kumaliza darasa la saba, aliendelea na masomo yake ya sekondari ya awali katika shule ya Lububu katika wilaya ya Nzega Mkoani Tabora, ambapo alisoma kwa muda wa miezi minne kutokana na sababu mbalimbali hakuweza kuendelea na masomo kwani alisoma miezi minne tu, kati ya miezi kumi na mbili aliyotakiwa kusoma.

Mwaka uliofutia, yaani mwaka 1996, alihamishiwa nchini Kenya ambapo kutokana na unataratibu wa elimu ya nchini Kenya alitakiwa kufanya maandalizi kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa muda wa mwaka mmoja na mwaka 1997, alianza kidato cha kwanza katika shule ya wavulana ya Isebania iliyoko kama kilometa mbili kutoka katika mpaka wa Sirari katika wilaya ya Kurya hadi mwaka 2000, ambapo alimaliza kidato cha nne katika shule hiyo.

Katika sanaa Ngelela alionekana kuwa na kipaji kikubwa jambo ambalo lilichangia kupata ruhusa kwa wazazi wake kwenda kusomea sanaa katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TASUBA)[dead link] ambapo alichukuwa stashahada yake ya sanaa. Baadaye Ngelela alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua Shahada yake ya kwanza na shahada ya uzamili ya sanaa za maonesho na sanaa za ufundi.

Huku akiwa anatuma maombi katika vyuo mbalimbali hatimaye alipata nafasi katika chuo cha sanaa Bagamoyo nchini Tanzania ambapo alikuwa akichukua stashahada ya sanaa kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kuhitimu masomo yake ya sanaa chuoni hapo alijiunga na chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alikuwa akichukua shahada ya Sanaa ya Maonesho na Sanaa ya Ufundi (Bachelor of Arts in Fine and Performing Arts) ambapo mwaka 2008, alitunukiwa shahada yake ya kwanza katika masula ya sanaa za maonesho na sanaa za ufundi.

Baada ya kumaliza elimu yake katika chuo kuku cha Dar es Salaam na kupata shahada yake, alianza kuchua shahada ya uzamili katika masuala hayo hayo ya sanaa, masomo aliyohitimu mwaka 2010.

. . . Edgar Ngelela . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Edgar Ngelela . . .

Previous post Primasia
Next post Uchambuzi namba