Audie Cornish

Audie N. Cornish[1] (alizaliwa Oktoba 9, 1979) ni mwandishi wa habari kutokea nchini Marekani. Kwa sasa ni muongoza kipindi cha NPR kwa jina la All Things Considered, pia ni mshiriki wa kioindi cha Pop Culture Happy Hour.[2] Hapo kabla alikuwa ni muendesha kipindi cha Profile kilichorushwa na kituo cha BuzzFeed News, kipindi cha mahojiano cha mitandaoni pekee kilichorushwa kwa msimu mmoja tu, pamoja na NPR Presents, kipindi cha mahojiano juu ya kazi, miradi na taratibu mbalimbali zilizolenga kuboresha utamaduni wa Kimarekani.[3]

. . . Audie Cornish . . .

Cornish alizaliwa jijini Randolph, Massachusetts, wazazi wake ni Wajamaika, na alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Randolph High School.[4][5]

Alihitimu elimu ya juu katika chuo kikuu cha Massachusetts-Amherst.[6] Wakati akiwa chuoni, alifanya kazi ya kujitolea katika kituo cha NPR[7][8] na kufanya kazi pia katika kituo cha redio cha chuoni WMUA.

Kazi za hapo awali zilihusisha uandishi wa Habari katika kituo cha NPR la WBUR, shirika la utangazaji na habari la Associated press la jijini Boston, na NPR kuhusiana na masuala ya majimbo kumi ya kusini mwa Marekani pamoja na yale Capitol Hill. Alishirikiana tuzo ya mshindi wa kwanza ya mwaka 2005 katika tuzo ya kitaifa ya uandishi wa kuelimisha (National Awards for Education Writing) juu ya mafanikio ya kitabaka baina ya jamii. Ni mjumbe wa Shirika la waandishi Habari weusi (National Association of Black Journalists).[9]

Kigezo:External media Mnamo Septemba 4, 2011, Cornish alichukua nafasi ya Liane Hansen wa NPR katika kipindi cha Weekend Edition Sunday. Hansen alitayarisha na kuendesha kipind hicho kwa zaidi ya miaka 20.

Mwishoni mwa mwaka 2011, Disemba 18 muendesha kipindi cha Weekend Edition, Cornish aliweka bayana kuwa ataacha kuendesha kipindi hicho na kuhamia katika kipindi cha All Things Considered ifikapo Januari 2012 wakati wa chaguzi za mwaka 2012, kipindi chake kilichukuliwa na mtangazaji mwingine kwa jina la Rachel Martin.[10] Imekuwa ikitajwa sababu ya kuondoka katika kipindi hicho kilisababishwa na mume wake kuwa sehemu ya wanaharakati katika kampeni ya Barack Obama.[11] Mnamo Januari 3, 2013, NPR ilitangaza kuwa Cornish atabakia kuwa muendesha kipindi hicho na Norris atarudi kama muandaaji taarifa wa kipindi.[12]

Mnamo Agosti 2017, Cornish alitangaza kuwa angeondoka NPR wakati atakapopata likizo ya uzazi.[13] Akiwa katika likizo hiyo, alichapisha mahojiano kadhaa katika jarida la The New York Times.[14][15]

All Things Considered ina wasikilizaji takribani milioni 14 kwa wiki.[2][3]

. . . Audie Cornish . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Audie Cornish . . .

Previous post Mwana wa Mungu
Next post Ықылас Дүкенұлы