Athroskopia

Athroskopia (pia huitwa upasuaji wa kifundo) ni upasuaji wa kuingilia kwa kiasi kidogo kabisa ambapo uchunguzi na wakati mwingine matibabu ya uharibifu ndani wa kifundo hutekelezwa kwa kutumia athroskopu, aina ya hadubini inayoingizwa ndani ya kifundo kupitia mkato mdogo. Taratibu za kiathroscopia zinaweza kutekelezwa ama kutathmini au kutibu hali nyingi za mifupa pamoja na gegedu sogezi zilizoachana, gegedu za uso zilizoachana, ujenzi upya wa kano ya kushikilia goti mbele , na kusawazisha gegedu zilizoharibika.

Picha:Performing shoulder arthroscopy.jpg
Mfano wa athroskopia ya bega. Daktari mpasuaji hutazama skrini ya video ambayo imeunganishwa kwa kamera ambayo imeingizwa ndani ya mwili, pamoja na vyombo vya kazi.

Athroscopia kuliko upasuaji wazi wa jadi ni kwamba kifundo hakihitajiki kufunguliwa kikamilifu. Badala yake, kwa mfano athroscopia ya kifundo cha goti, mikato miwili midogo hufanywa – mmoja kwa ajili ya athroskopu na mmoja kwa ajili ya vyombo vya upasuaji vitakavyotumika katika pengo la goti na kuondoa funiko la goti kabisa. Hii hupunguza muda wa kupona na inaweza kuongeza kiwango cha mafanikio ya upasuaji kutokana na kiwewe cha chini kwenye tishu unganifu. Ni muhimu hasa kwa wanariadha wa kulipwa, ambao hujeruhi kifundo cha goti mara kwa mara na wanahitaji muda mfupi wa uponyaji. Kuna pia upungufu wa makovu, kwa sababu ya mikato midogo. Ugiligili wa kumwagiliwa hutumika kutanua kifundo na kutengeneza nafasi ya kupasulia. Wakati mwingine ugiligili huu huvuja hadi kwenye tishu laini zilizo karibu na kusababisha uvujaji na uvimbe wa giligili.

Vyombo vya upasuaji vinavyotumika ni vidogo kuliko vyombo vya jadi. Madaktari wapasuaji hutazama eneo la kifundo kwenye skrini ya video, na wanaweza kutambua au kurekebisha tishu za kifundo zilizoachana, kama vile kano na meniski au gegedu.

Inawezekana kitaalam kufanya uchunguzi wa kiathroscopia wa karibu kila kifundo katika mwili wa binadamu. Vifundo vinavyochunguzwa na kutibiwa kwa kutumia athroscopia aghalabu huwa ni vya goti, bega, kiwiko cha mkono, kifundo cha mkono, tindi la mguu, mguu, na nyonga.

. . . Athroskopia . . .

Profesa Kenji Takagi wa Tokyo amesifiwa tangu jadi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kwanza wa athroskopia ya kifundo cha goti la mgonjwa mwaka wa 1919. Alitumia sistoskopu ya 7.3 mm kwa athroskopia zake za kwanza. Hivi karibuni imegunduliwa kuwa daktari wa Kideni Severin Nordentoft alitoa taarifa juu ya athroskopia za kifundo cha goti mwaka wa 1912 katika taarifa juu ya athroskopia ya goti ya pamoja mapema 1912 katika Kumbukumbu za Mkutano maalum wa 41 wa Shirika la Madaktari wapasuaji la Ujerumani huko Berlin. [1] Alibatiza utaratibu huo (kwa Kilatini) athroskopia genu. Nordentoft alitumia mchanganyiko wa chumvi tasa au wa asidi boriki kama chombo chake cha macho na aliingia ndani ya kifundo kwa kutumia pota kwenye mpaka wa nje wa kilegesambwa. Hata hivyo, si wazi ikiwa uchunguzi huu ulikuwa utafiti wa anatomia ya wagonjwa waliofariki au wanaoishi.

Kazi za kutagulia katika taaluma ya athroskopia zilianza miaka ya 1920 na kazi ya Eugen Bircher. [2] Bircher alichapisha majarida kadhaa katika miaka ya 1920 kuhusu matumizi yake ya athroskopia ya goti kwa madhumini ya kutambua ugonjwa. [2] Baada ya kutambua tishu zilizoachana kwa kutumia athroskopia, Bircher alitumia upasuaji wazi katika kuondoa au kurekebisha tishu zilizokuwa zimeharibika. Awali, alitumia thoracolaparoscopu ya Jacobaeus ya umeme kwa ajili ya taratibu zake za kutambua ugonjwa, ambayo ilionyesha mtazamo usio dhahiri wa kifundo. Baadaye, alifafanua mtazamo wa utofautishaji maradufu wa kuboresha hali ya kuonekana. [3] Bircher aliacha uhadubini mnamo mwaka wa 1930, na kazi yake ilitelekezwa sana kwa miongo kadhaa.

Wakati Bircher anakumbukwa mara kwa mara kama mvumbuzi wa athroskopia ya goti, [4] daktari mpasuaji wa Kijapani Masaki Watanabe, MD anapokea sifa kuu kwa kutumia athroskopia kwa upasuaji rekebishi. [5][6] Watanabe alitiwa moyo na kazi na mafundisho ya Dr Richard O’Connor. Baadaye, Dr. Heshmat Shahriaree alianza kufanya majaribio ya njia za kukata vipande vya meniski. [7]

Athroskopu ya kwanza kutumika iliundwa kwa ushirikiano na watu hawa, na walifanya kazi pamoja kupiga picha wa kwanza wa rangi wa hali ya juu wa ndani ya kifundonisho[8] Taaluma ilinufaika sana kutokana na maendeleo ya teknolojia, hasa maendeleo katika nyuzi za optiki za kunyumbulika miaka ya 1970 na 1980.

Zuia usemi

. . . Athroskopia . . .

This article is issued from web site Wikipedia. The original article may be a bit shortened or modified. Some links may have been modified. The text is licensed under “Creative Commons – Attribution – Sharealike” [1] and some of the text can also be licensed under the terms of the “GNU Free Documentation License” [2]. Additional terms may apply for the media files. By using this site, you agree to our Legal pages . Web links: [1] [2]

. . . Athroskopia . . .

Previous post Historia ya maeneo ya Pasifiki
Next post Primasia